Shughuli ya kuhesabu kura inatarajiwa kuanza leo asubuhi nchini Sudan baada ya siku nne za upigaji kura katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kumrejesha madarakani Rais Omar al Bashir ambaye ameliongoza taifa hilo kwa miaka 25. Bashir mwenye umri wa miaka 71 anakabiliwa na ushindani mdogo baada ya vyama vikuu vya kisiasa kuususia uchaguzi huo wa Rais na wagombea wawili kujiondoa siku ya Jumatano baada ya uchaguzi kurefushwa kwa siku moja zaidi. Ujumbe wa waangalizi wa umoja wa Afrika umetoa taarifa baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa na kusema idadi ndogo ya wapiga kura ilijitokeza kushiriki katika shughuli hiyo.